wavuvi

Malengo

 • Kuwakinga wavuvi dhidi ya majanga kwa kuwapa mafao yote Yatolewayo na NSSF
 • Kuwapa wavuvi na familia zao matibabu ya bure ili wawe na afya bora ya kuweza kuzalisha kwa ufanisi zaidi.
 • Kusaidiana na serikali kupunguza umaskini kwa jamii.kujenga Kizazi kisicho tegemezi kwa kutoa pensheni ya uzee, urithi na Ulemavu na kupambana na umasikini kwa ujumla.
 • Kuwawezesha wavuvi kupata mikopo ya riba nafuu sana kwa ajili ya kununulia pembejeo,kusomesha watoto wao, na shughuli nyingine za maendeleo.
 • Kunusuru kipato ambacho wangekitumia katika matibabu na badala yake wakitumie kujiendeleza kiuchumi
 • Kuwawezesha wavuvi kupata mafao ya pensheni wakati watakapokuwa wazee na kushindwa kuendelea na uvuvi.
 • Kuwaunganisha wavuvi kwa pamoja ili watambue kuwa wapo kwenye ajira yenye tija kwao, na hivyo wazidi kuithamini na kuiendeleza na hatimaye kuleta kipato kwao na kwa taifa kwa ujumla.
 • Kuwajengea wavuvi utamaduni wa kujiwekea akiba ili iweze kuwasaidia nyakati ambapo hakuna uzalishaji.

Wanaohusika Na Mpango Huu

 • Wanachama wote waliojiunga na vikundi shirikishi vya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi (BMU) au vyama vingine vyovyote vya uvuvi
 • Mvuvi mmojammoja ilimradi awe na uhakika wa kuweza kuchangia japo Tshs. 20,000/- na zaidi kwa kila mwezi
 • Watu wote wanaojishughulisha na biashara zote za uvuvi ikiwemo ununuzi wa samaki, usafirishaji, usindikaji, uongezaji thamani (Fish prossessing), uuzaji wa samaki na yale yote yatokanayo na uvuvi wa samaki ambao hawapo katika ajira rasmi.
 • Watu wote wanaojishughulisha na uvuvi,ufugaji wa samaki ,pamoja na wale wote wanaojishughulisha na biashara zitokanazo na shughuli zilizotajwa hapo juu.

ULIPAJI MICHANGO:

 • Mwanachama wa sekta ya uvuvi atapaswa kulipa kiwango chochote ilimradi kisiwe chini ya (Tshs. 20,000/-kwa sasa.)
 • Michango hiyo itaanza tu mara mwanachama atakapoandikishwa.
 • Michango hiyo hulipwa kila mwezi bila kuruka. Mwanachama akiruka mwezi/miezi itambidi alipie miezi hiyo ili huduma/mafao hasa ya matibabu yaendelee.
 • Michango itapokelewa katika ofisi yoyote ya NSSF nchini na risiti itatolewa.
 • Michango hiyo pia inaweza kulipwa kupitia vyama vyao kwa namna ambayo watakubaliana wanachama,na NSSF sehemu husika.
 • Michango inaweza kuwasilishwa kwa mfumo wa simu M-PESA, TIGO PESA, NA AIRTEL MONEY kwa namba zitakazotolewa.
 • Mwanachama anaweza kulipa kwa miezi ya mbele,kwa msimu,au kwa mwaka mzima.

 

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1