Malengo

 • Kutoa mafao yote yatolewayo na NSSF kwa wanachama wa sekta ya Kilimo.
 • Kuwapa wakulima na familia zao matibabu ya bure ili wawe na afya bora ya kuweza kendesha kilimo bora
 • Kusaidiana na serikali kupunguza umaskini kwa jamii.
 • Kuwawezesha wakulima kupata mikopo ya riba nafuu sana kwa ajili ya kununulia pembejeo,kusomesha watoto wao,na shughuli nyingine za maendeleo.
 • Kunusuru kipato ambacho wangekitumia katika matibabu na badala yake wakitumie kujiendeleza kiuchumi na kuweza kurejesha mikopo popote walipokopa.
 • Kuwawezesha wakulima kupata mafao ya pensheni wakati watakapokuwa wazee na kushindwa kuendelea na kilimo.

 Wanaohusika na Mpango huu

 • Wakulima wote waliojiunga na vyama vya msingi vya mazao (AMCOS) au vyama vingine vyovyote vya ushirika.
 • Mkulima mmojammoja ilimradi awe na uhakika wa kuweza kuchangia japo Tshs. 20,000/- na kuendelea kwa kila mwezi
 • Watu wote wanaojishghulisha na biashara zote za kilimo ikiwemo ununuzi wa mazao, usafirishaji, usindikaji, uongezaji thamani (Agri prossessing), uuzaji wa mazao na yale yote yatokanayo na mazao ya kilimo.
 • Watu wote wanaojishughulisha na ufugaji wa wanyama,nyuki, uwindaji,na uvuvi,pamoja na wale wote wanaojisghulisha na biashara ya mazao yatokanayo na shughuli zilizotajwa hapo juu.
 • Wanachama walio katika mifuko mingine ila wakapenda kujiunga kwa mfumo wa hiari ili kupata mafao yatolewayo na NSSF. Wanachama wanaopata
 • pensheni ya NSSF na wakawa radhi kukatwa asilimia sita(6%) ya pensheni yao ili kuweza kupata huduma ya matibabu.

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1