Malengo

Kuongeza wanachama na kukidhi mahitaji ya wanachama.

Walengwa wa Mpango

Mpango unalenga kufaidisha wanachama wa Mfuko kupitia SACCOS zinazofanya kazi Tanzania.

Madhumini ya Mpango

 • Kusaidia Miradi ya Maendeleo
 • Kusaidia Elimu

Sifa zinazotakiwa

 • Mwanachama
  • Lazima awe mwanachama wa NSSF kwa muda usiopungua miezi sita na lazima awe mwanachama hai katika michango; na
  • Anapaswa kuomba mkopo kupitia SACCOS ambayo yeye ni mwanachama.

SACCOS Scheme

 • lazima iwe imesajiliwa kihalali na uendeshaji wake uwe Tanzania kwa miaka si chini ya mitatu;
 • inapaswa kuwasilisha Taarifa za fedha zilizokaguliwa kwa miaka mitatu iliyopita;
 • inapaswa kuwasilisha orodha ya wasimamizi waliothibitishwa na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika; na
 • kuwasilisha nguvu za ukopaji za SACCOS husika na sheria zake, kikomo cha ukopaji kilichowekwa katika Mkutano wake Mkuu na maamuzi ya Bodi

Kuhusu ukopaji.

Taratibu za Maombi

 • Mwanachama wa NSSF anapaswa kuomba mkopo kupitia SACCOS yake husika;
 • SACCOS inapaswa kupokea,kutathmini na kuidhinisha maombi ya mkopo unaohitajika katika kipengele (a) hapo juu kwa kuzingatia   sheria zake za kukopesha;
 • Juu ya msingi wa maombi ya mkopo yaliyopitishwa kama ilivyoonyeshwa katika kipengele (b) hapo juu, SACCOS itakusanya orodha rasmi za maombi ya mkopo / mikopo na koumba mkopo mmoja kutoka NSSF orodha ya waombaji lazima iambatanishwe; na
 • Maombi yote kutoka SACCOS lazima yapitie ofisi za mkoa za NSSF kwa ajili ya tathmini ya awali na baadaye kuwasilishwa Ofisi ya NSSF Makao Makuu kwa tathmini ya kina.

Mipaka ya Mkopo

Kwa SACCOS, kiwango cha chini cha mkopo ni million 50.0 na kiwango cha juu ni billion 1.0 Hata hivyo, kiasi hicho kiwe kisichozidi 50% ya jumla ya rasilimali za SACCOS. Kikomo cha kukopa kwa ajili ya wanachama kitawekwa na SACCOS husika.

Riba za Mikopo

Kiwango cha riba kwa mikopo kitatumia msingi wa kiwango cha riba ya dhamana fungani za serikali za miaka miwili na mitano kwa miaka miwili na mitano, pamoja na nyongeza ya asilimia 1.5%. SACCOS itaruhusiwa kuongeza faida isiyozidi 3% juu ya kiwango cha NSSF. Kwa kuanzia, viwango vifuatavyo vitahusika:-

 • Mikopo ya marejesho kwa miaka miwili = 9.32%kwa mwaka
 • Mikopo ya marejesho kwa miaka mitano =10.68% kwa mwaka

 Dhamana ya Mikopo

Mikopo itakuwa itawekewa dhamana ya 100%. Dhamana inaweza kuwa:-

 • mali zisizohamishika za SACCOS husika;
 • Udhamini kutoka benki au mwajiri kwa kiasi cha mkopo na riba husika;
 • Bima ya mkopo na riba husika;
 • amana za muda maalum; au
 • mchanganyiko wa yaliyotajwa hapo juu.

Bima ya Mikopo

Mikopo yote iliyotolewa kwa SACCOS yoyote kwa madhumuni ya kukopesha kwa wanachama wa NSSF itakatiwa bima katika kipindi chote cha mkopo na mkopaji atachukua gharama ya bima.

Urejeshaji wa Mkopo

 • mikopo italipwa kwa kipindi cha miaka kati ya 2 na 5.
 • Ulipaji wa mikopo utakuwa ni kila mwezi;

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1