Malengo

  • Kuwakinga wachimbaji wadogo dhidi ya majanga kwa kuwapa mafao yote yatolewayo na NSSF.
  • Kuwapa wachimbaji wadogo na familia zao matibabu ya bure ili wawe na afya bora ya kuweza kuzalisha kwa ufanisi zaidi.
  • Kusaidiana na serikali kupunguza umaskini kwa jamii,kujenga kizazi kisicho tegemezi kwa kutoa pensheni ya uzee,urithi na ulemavu,na kupambana na umaskini kwa ujumla.
  • Kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata mikopo ya riba nafuu sana kwa ajili ya kununulia vitendea kazi,kusomesha watoto wao,na shughuli nyingine za maendeleo.
  • Kunusuru kipato ambacho wangekitumia katika matibabu na badala yake wakitumie kujiendeleza kiuchumi na kuweza kurejesha mikopo popote walipokopa.
  • Kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata mafao ya pensheni wakati watakapokuwa wazee na kushindwa kuendelea na kazi hiyo.
  • Kuwaunganisha wachimbaji wadogo kwa pamoja ili watambue kuwa wapo kwenye ajira yenye tija kwao, na hivyo wazidi kuithamini na kuiendeleza na hatimaye kuleta kipato kwao na kwa taifa kwa ujumla.
  • Kuwajengea wachimbaji utamaduni wa kujiwekea akiba ili iweze kuwasaidia nyakati ambapo hakuna uzalishaji.

Wanaohusika na Mpango huu

  • wachimbaji wadogo wote waliojiunga na vyama vya wachimbaji vya mikoa, (REMAS) au vyama vingine vyovyote vya ushirika wenye leseni na wasio na leseni
  • Mchimbaji mmojammoja ilimradi awe na uhakika wa kuweza kuchangia japo Tshs. 50,000/- na kuendelea kwa kila mwezi
  • Watu wote wanaojishughulisha na biashara zote za madini ikiwemo ununuzi wa madini,,usafirishaji,uongezaji thamani,uuzaji na yale yote yatokanayo na madini hayo ambao hawapo katika ajira rasmi.

Ulipaji Michango:

  • Mwanachama wa sekta ya madini atapaswa kulipa kiwango chochote ilimradi kisiwe chini ya (Tshs. 50,000/- kwa sasa).
  • Michango hiyo itaanza tu mara mwanachama atakapoandikishwa.
  • Michango hiyo hulipwa kila mwezi bila kuruka. Mwanachama akiruka mwezi/miezi itambidi alipie miezi hiyo ili huduma/mafao hasa ya matibabu yaendelee.
  • Michango itapokelewa katika ofisi yoyote ya NSSF nchini na risiti itatolewa.
  • Michango hiyo pia inaweza kulipwa kupitia vyama vyao kwa namna ambayo watakubaliana wanachama,viongozi wao, na NSSF sehemu husika.
  • Michango inaweza kuwasilishwa kwa mfumo wa simu M-PESA, TIGO PESA,NA AIRTEL MONEY kwa namba zitakazotolewa.
  • Mwanachama anaweza kulipa kwa miezi ya mbele,kwa msimu,au hata kwa mwaka mzima.

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1