hiari

Hiari Scheme Ni Nini

Ni Skim mahsusi iliyoanzishwa na shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii kwa nia ya kutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa watu walio katika sector isiyo rasmi, waliojiajiri wenyewe ,na wale walio katika mifuko mingine na wakapenda kujiunga kwa hiari.

Wanaohusika Na Mpango Huu

 • Wanachama wote waliojiunga katika vikundi vya uzalishaji mali
 • Mwanachama mmojammoja ilimradi awe na uhakika wa kuweza kuchangia japo Tshs. 20,000/- na kuendelea.
 • Wanachama wote walio chini ya SACCOS na vyama vya ushirika nchini
 • Wanachama wote wasio katika mfuko wa hifadhi ya jamii kisheria
 • Wanachama walio katika mifuko mingine ila wakapenda kujiunga kwa mfumo wa hiari ili kupata mafao yatolewayo na NSSF.
 • Wanachama wanaopata pensheni ya NSSF na wakawa radhi kukatwa asilimia sita(6%) ya pensheni yao ili kuweza kupata huduma ya matibabu
 • Wakulima
 • Wachimbaji wadogo wa madini
 • Wavuvi

Uandikisha Wa Uanachama Wa Hiari

 • Uandikishaji katika ofisi yoyote ya NSSF nchini.
 • Uandikishaji katika maeneo ya biashara/shughuli zao kwa kuwaita maofisa wa NSSF
 • Uandikishaji ni kwa njia ya Computer na kadi ya ki-electronikia yenye namba ya uanachama hutolewa.(SMART CARD)

Uchangiaji Kwa Mwananchama Wa Hiari

 • Mwanachama wa hiari/sekta isiyo rasmi atapaswa kulipa kiwango chochote ilimradi kisiwe chini ya Tshs. 20,000/- kwa mwezi na wale wachimabaji wadogo sh.50,000/-
 • Michango hiyo itaanza tu mara mwanachama atakapoandikishwa.
 • Michango hiyo hulipwa kila mwezi bila kuruka. Mwanachama akiruka mwezi/miezi itambidi alipie miezi hiyo ili huduma/mafao hasa ya matibabu yaendelee.
 • Michango itapokelewa katika ofisi yoyote ya NSSF nchini na risiti itatolewa.
 • Michango inaweza kuwasilishwa kwa mfumo wa simu M-PESA, TIGO PESA, NA AIRTEL MONEY kwa namba zitakazotolewa.

Faida Za Kuwa Mwanachama Wa Hiari

Mafao ya matibabu ya bure kwawanachama wa NSSF

Sifa

 • Michango ya kuanzia miezi mitatu tu (3)

Wahusika

 • Mume, Mke na Watoto 4 wenye umri usiozidi miaka 18 na 21 kwa wanaosoma
 • Wastaafu watakaotaka huduma hii baada ya kustaafu.

Huduma za matibabu,

 • Kumuona daktari na huduma za uchunguzi
 • Upaasuaji
 • Huduma za dawa
 • Huduma za rufaa kwenda hospitali za juu.

Mipaka katika utoaji wa huduma

 • Matibabu ya dharura nje ya vituo/hospitali aliyojiandikisha mwanachama.
 • Wanachama wanaosafiri kikazi zaidi ya mara nne kwa mwaka nje ya mikoa yao
 • Kulazwa zaidi ya siku 42 kwa mwaka

Huduma za matibabu yatasitishwa endapo:

 • Mwanachama Akifariki,
 • Kuachishwa au kuacha kazi kwa mwanachama
 • Kustaafu kwa umri
 • Kutowasilisha kwa michango kwa miezi mitatu na
 • Kufikia umri wa zaidi ya miaka 18 au 21 kwa watoto wa mwanachama

Jinsi ya kujiandikisha tembelea ofisi za NSSF zilizopo nchini kote ukiwa na kadi yako ya uanachama pamoja na picha za pasipoti tatu

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1