Wajibu wa Kulipa Michango
Jukumu la kuhakikisha michango ya wanachama inalipwa kwa wakati ni la mwajiri mwenyewe na wafanyakazi wake. Hata hivyo ili kuhakikisha waajiri na wanachama wanajiandikisha na kulipa michango kwa wakati Shirika hutumia pia wakaguzi wake ambao hufanya ukaguzi kwa waajiri kila mara inapobidi.