Aina za Ukaguzi
Kuna aina kuu tatu za ukaguzi ambao hufanywa na wakaguzi wa shirika katika kuhakikisha waajiri na wanachama wanatekeleza wajibu wao kisheria.
Ukaguzi wa Kawaida (Routine)
Huu ni ukaguzi unaofanyika mara mbili kwa mwaka kwa kila mwajiri. Katika ukaguzi huu mwajiri anawajibika kutoa taarifa zote zinazohusiana na wafanyakazi wake kwa ajili ya ukaguzi. Mkaguzi anayehusika atatoa taarifa rasmi ya kufanya ukaguzi huo kabla ya siku ya ukaguzi.
Ukaguzi Fuatilizi (follow up)
Huu ni ukaguzi wa mara kwa mara unaofanywa kwa lengo la kufuatilia jambo maalum kama michango isiyolipwa, adhabu iliyotozwa, hundi iliyorudishwa benki, uandikishaji wa wanachama, n.k.
Ukaguzi Chunguzi (Survey)
Huu ni ukaguzi unaofanywa kwa lengo la kugundua waajiri wasiojiandikisha katika Shirika ili kutimiza wajibu wao wa kisheria.
Adhabu
Iwapo mwajiri atachelewesha michango zaidi ya mwezi mmoja baada ya mwezi wa mishahara asilimia 5 ya mchango husika hutozwa kama adhabu kwa kila mwezi uliocheleweshwa.