News Archive

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limejiunga katika mfumo wa Malipo ya Serikali Kieletroniki (GePG) ambapo umeanza kutumika mwishoni mwa mwezi wa tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake Dar es Salaam, jana, Meneja Kiongozi, Mahusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele alisema huduma hiyo itaongeza ufanisi kwa Shirika.

Pia, itamuwezesha mwajiri kulipia michango ya wafanyakazi wake popote alipo kwa kutumia simu za mikononi au huduma za kibenki.

“Shirika limeingia katika mfumo wa malipo ya serikali kieletroniki, hivyo tunawaomba waajiri wote kulipa michango ya wafanyakazi wao kwa kutumia mfumo huo,” alisema Lulu.

Alisema ili mwajiri aweze kulipia kupitia mfumo wa GePG anapaswa kujiandikisha na kupewa namba “Control number” ambayo itatolewa na Shirika.

Lulu alisema waajiri wanatakiwa kuwasiliana na ofisi za NSSF zilizo karibu nao kwa kupatiwa maelezo zaidi.

Alisema waajiri wanatakiwa kuwasilisha taarifa muhimu katika Shirika kama barua pepe, jina la mfanyakazi anayehusika na malipo, namba ya simu ya mkononi ya kampuni, lengo ni kupata mrejesho kwa haraka baada ya malipo kukamilika.

Lulu alifafanua zaidi kwamba huduma hiyo itaongeza ubora na uwajibikaji wa pande zote mbili na kwamba mwajiri akilipia anapaswa kuwasilisha nakala laini ya jedwali la michango.

Alisema jadwali hilo litaonesha michango ya kila mfanyakazi mmoja mmoja inayowasilishwa kwenye Shirika hilo ili kusaidia kuingiza michango ya mwanachama.

Lulu alisema awali, waajiri walikuwa wanawasilisha michango kwa kutumia hundi au fedha tasilimu.

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4