News Archive

Bakhresa alisema hayo jana, ofisini kwake Dar es Salaam, alipokutana na uongozi wa Shirika hilo ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, William Erio, ambaye kwa kushirikiana na timu yake walifanya ziara katika shamba la Bagamoyo Sugar lililopo Makurunge, Bagamoyo mkoani Pwani kwa ajili ya kujifunza.

 

Shamba hilo lenye ukubwa wa hekta 10,000 sawa na ekari 25,000, linamilikiwa na kampuni ya Bakhresa, ambalo litajengwa kiwanda cha sukari.

Bakhresa Bakhresa alimshukuru Erio na timu yake kwa kwenda ofisini kwake na kuzungumza.

“Nakushukuru wewe na timu yako kwa kuja maana tumepeana  uzoefu wa kutosha na tumepeana maarifa mengi na kuzungumza mengi,” alisema.

Aliahidi kuendelea kukutana na uongozi wa Shirika hilo kwa ajili ya kuzungumza mambo mbalimbali, ambapo alisisitiza kwamba yupo tayari muda wowote kukutana nao.

Kwa upande wake, Erio Erio alimshukuru Bakharesa kwa namna walivyopatiwa maelezo mazuri walipotembelea shamba hilo kwa ajili ya kujifunza.

“Tunakushukuru kwa nasaha zako, uzalendo wako na kukubali kutusikiliza na kubadilishana mawazo katika maeneo ambayo yatafanikisha uwekezaji ambao utafanikiwa na kuleta tija kwa taifa,” alisema.

Erio alimshukuru mfanyabiashara huyo kwa uwekezaji wake mkubwa katika viwanda vyake kwenye maeneo 17 tofauti, ambapo NSSF wanapata faida kwani wafanyakazi wa kampuni hizo ni wanachama wa Shirika hilo.

Alifafanua kwamba lengo la ziara hiyo ni kujifunza uzalishaji wa miwa na namna ya uendeshaji wa kiwanda cha sukari, ambapo NSSF kupitia kampuni yake ya Mkulazi Holding na Jeshi la Magereza wameanzisha kiwanda cha miwa katika Gereza la Mbigiri mkoani Morogoro.

Erio alisema wamepata fursa ya kutembelea baadhi ya viwanda vya sukari kwa ajili ya kujifunza, lakini tofauti ni kwamba Bagamoyo Sugar wanaanza moja kama wao.

Alisema viwanda vingine vilikuta miundombinu ilishajengwa na serikali, lakini baada ya ubinafsishaji walivinunua na kuviimarisha zaidi.

“Sisi tunaona uzoefu wa Bagamoyo Sugar na wa kwetu unafanana hii ni sehermu sahihi ya kujifunza na kuona wenzetu wanafanyaje na sisi tufanyaje, tumejifunza mengi ikiwemo tafiti zao walizaofanya,” alisema.

Alisema miongoni mwa mambo waliyojifunza ni namna ya kuhifadhi maji, kudhibiti mafuriko ya maji kwa maana ya kuyahifadhi, namna walivyojipanga katika kununua vifaa kwamba katika kudhibiti gharama watanunua wao wenyewe, lakini wamewaeleza wakati watakapoanza ni muhimu miwa ikawa ni ya shamba lao wenyewe.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa NSSF alisema wataendelea kuwa na ushirikiano wa muda mrefu na kiwanda hicho.

Kwa mujibu wa Erio, Shirika lina majukumu makubwa manne ambayo ni kuandikisha wanachama, kukusanya michango toka kwa wanachama, kuwekeza na kulipa mafao kwa wahusika wanapotimiza masharti wanapostaafu.

Alisema ujenzi wa kiwanda cha sukari ni njia moja wapo ya uwekezaji ambao ukifanywa vizuri unatija kubwa kwa taifa, jamii na Shirika.

Erio alisema uwekezaji wa kiwanda una manufaa mengi ikiwemo kupata mapato, watapunguza uhitaji wa sukari kutoka nje, wataiwezesha serikali kuokoa fedha za kigeni ambazo zinatumika kuagiza sukari na fedha hizo zitatumika kwenye mambo mengine.

Alisema  uwekezaji huo wa kiwanda pia utasababisha watu kupata ajira, kwamba watapata wanachama wapya ambao wataleta michango na kuuwezesha mfuko kukuwa.

Mkuu wa Mradi wa Bagamoyo Sugar, Hosein Sufiani, alisema eneo la mradi lina ukubwa wa hekta 10,000 ambalo walipewa na Rais Dk. John Magufuli, mwaka 2016.

Alisema wamefarijika kukutana na uongozi wa NSSF na kujadiliana kwa jinsi gani waendeleze miradi ya aina hiyo ambayo itakuwa na tija kwa taifa.

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4