News Archive

Wanachama na wadau wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakumbushwa kupiga simu bure ili kupata huduma kwa wakati, mwanachama anaweza akawasilisha malalamiko, maulizo na maoni.

Shirika limesema mwanachama atapiga namba ya simu bure 0800756773 kuanzia saa 2.30 asubuhi hadi saa 10.30 jioni, Jumatatu hadi Ijumaa.

 

“Shirika linaendelea kuwajali wanachama na wadau wake, hivyo kama mwanachama akipiga namba hiyo hatopata gharama zozote za kupiga simu.”

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele, alisema kwa Upande wa NSSF tunasema mwanachama kwanza.Tumekuja na utamaduni wa kumjali mwanachama, NSSF ipo kwa sababu ya wanachama hivyo kupata huduma ni haki yake, mwanachama anaweza
akawasilisha malalamiko yake, maswali, maoni na kupata taarifa zake za michango kupitia namba ya simu ya huduma kwa wateja.

Pamoja na huduma ya simu mwanachama anaweza akawasiliana na Shirika kupitia barua pepe This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Lulu alisema Shirika linapenda kuwahakikishia wanachama na wadau kwamba litaendelea kuboresha mifumo yake ya utendaji kazi na utoaji huduma kwa wanachama ili kuboresha na kurahisisha huduma kwa wateja.

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4