News Archive

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Charles Itembe, amekutana na wenye hisa wakubwa wa benki hiyo, ambao ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF, Hosea Kashimba na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF, William Erio.

PSSSF inamiliki asilimia 62 ya Benki ya Azania, wakati NSSF inamiliki asilimia 35, hivyo kwa ujumla wake mashirika hayo yanamiliki benki hiyo kwa asilimia 97, ambao ndio wamiliki wakubwa wa Benki hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya benki ya Azania, yaliyopo katika jengo la Mawasiliano, barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam, Itembe, alisema wanahisa hao walifanya ziara Azania ili kupata kufahamu mchakato unaoendelea wa kuchukua mali na madeni ya bank M.

Bwana Itembe aliwapatia maelezo kuhusu hatua zilizofanyika na matarajio ya baadae kwa wenye hisa hao kwani wamefanya uwekezaji mkubwa.

Mkurugenzi huyo alisema ni vizuri kwa wenye hisa hao kufahamu namna Benki ya Azania itakavyofanyakazi baada ya kuchukua Bank M.

Ikumbukwe Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliamua kuhamisha kwa mujibu wa sheria mali na madeni ya Benki M kwenda Azania Benki Ltd.

Hivyo, kwa sasa BoT na Azania wanaendelea kuandaa taratibu za kisheria za kuhamisha mali na madeni kwenda Azania.

BoT ilikubali Benki M ichukuliwe na Azania kwa ajili ya kuiendesha, ambapo kwa sasa mchakato huo upo hatua za mwisho ili benki hiyo iwe ya Azania moja kwa moja.

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4