Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio amefanya mazungumzo na Menejimenti ya baadhi ya Taasisi tatu za Kibenki hapa nchini ambazo ni NMB,CRDB na UBA kwa lengo la kuendeleza na kukuza mahusiano ya kibiashara.
Katika mkutano huo wameweza kuzungumza masuala mbali mbali yanayolenga kuimarisha ushirikiano utakaowezesha kukuza maendeleo katika sekta ya uchumi kupitia Benki zao na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF.
Wakurugenzi wakuu hao ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bwana Charles Kimei,Bwana Usman Imam Isiaka Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker.
Viongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na viongozi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao kwenye ofisi za makao makuu ya NSSF ,katikati Mkurugenzi mkuu wa NSSF Bwana William Erio na pembeni yake ni Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Charles Kimei na pembeni ni viongozi mbalimbali wa CRDB na NSSF.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA ,Bwana Usman Imam Isiaka akielezea jambo wakati wa mazungmzo yake na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio katika ofisi za makao makuu ya NSSF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya NMB Bi.Ineke Bussemaker akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Bwana Michael Mungure amabaye ni MKuu wa kitengo cha akaunti na malipo(NMB), wa kwanza kulia ni Richard Mtapa ambaye ni Meneja Mwandamizi wa Taasisi za Serikali(NMB).