News Archive

Mkurugenzi MKuu  wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Ndugu William Erio amesema kwa sasa Shirika  liko katika hatua za mwisho wa kuweka mfumo wa utambuzi wa vyombo vya usafiri ili kuhakikisha mapato ya daraja yanaongezeka  kutokana na uhalisia wa tozo halisi ya magari.

 

Ndugu William Erio amesema kuwa TRA ina mfumo madhubuti wa utambuzi wa aina za magari na thamani, mfumo huo utaunganishwa moja kwa moja na Mfumo wa mamlaka hiyo ili kuhakikisha kila gari linalopita daraja la Nyerere linatozwa  tozo kulingana na aina na uzito wa kila  gari

Alisema awali  Shirika lilikuwa katika hatua za mwisho kwa ajili ya kumpata mkandarasi katika sekta binafsi lakini baadae Shirika lilibaini madhaifu katika mchakato huo hivyo kuamua kutumia wakala wa serikali ili kuweza kufanikisha kazi hiyo na kwa sasa mchakato wa manunuzi upo katika hatua za mwisho.

Kwa kutumia mfumo huo wa kisasa Shirika litaweza kukusanya mapato ya hadi bilioni moja kwa mwezi ikilinganishwa kwa sasa ambapo mapato yanifika zaidi ya milioni 800 kwa mwezi.

Hayo aliyazungumza wakati wa ziara ya Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Sera, Bunge, na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea kujua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya kilomita mbili inayounganisha daraja la Nyerere na maeneo mengine ya Wilaya ya Kigamboni.

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4