News Archive

Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF) limetoa msaada wa vifaa tiba katika hospitali ya Mkoa wa Temeke kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma katika Hospitali hiyo.

 

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Kaimu Meneja kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke Ndugu Barnabas Ndunguru amesema msaada huu ni moja ya jukumu la shirika za kurudisha fadhila kwa jamii katika kuisaidia serikali kwenye juhudi za kuboresha sekta ya afya Nchini.

Amesema, sekta ya afya nchini imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo za ukosefu wa vifaa tiba jambo ambalo linapelekea baadhi ya hospitali kushindwa kutoa huduma kwa ufanisi.

Ameongeza kuwa suala uboreshaji sekta ya afya nchini siyo jukumu la serikali peke bali ni la Watanzania wote kwa ujumla katika kuhakikisha wansaidia serikali katika kuimarisha sekta ya afya .

 

Vifaa hivyo vilivyotolewa vinathamani ya shilingi milioni tano ambapo vitaweza kuondoa upungufu uliopo kwa sasa huku meneja akisema kuwa NSSF itaendelea kusaidia katika sekta hiyo ya afya.

Kwa upande wake katibu wa afya wilaya ya Temeke bi Lilian Mwanga ameishukuru NSSF kwa msaada walioutoa na kuwa wanasaidia juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya Afya.

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4