News Archive

Shirika la Taifa la Hifahdi ya Jamii (NSSF) imetoa msaada wa Kompyuta tano zenye thamani ya Sh. Milioni 9, katika Kituo cha Afya cha Magomeni kwa lengo la kusaidia kutunza kumbukumbu za wagonjwa.

 

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Ofisa Mwandamizi wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Theopista Muheta, alisema wameamua kufanya hivyo ili kusaidia wagonjwa ambao ni wanachama wao wanaotibiwa katika Hospitali hiyo kuweza kupata huduma nzuri kutokana na kuwepo na taarifa sahihi.

Alisema Hospitali hiyo ni moja ya Hospitali ambazo wanachama wao wanatibiwa kwa kiwango kikubwa hivyo wametoa Kompyuta kwa ajili ya kuwezesha
wahudumu kuhifadhi taarifa hizo Kielectoniki tofauti na sasa wanavyotunza katika makaratasi.

“Wanachama wetu wengi wanatibiwa hapa, tumekuwa tukitoa misaada mbalimbali katika vituo vya afya kwasababu wanachama na wastaafu wa NSSF ndipo wanapotibiwa, kunavyokuwa na taarifa sahihi huduma zinakuwa bora Zaidi” alisema Muheta

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni Aziz Msuya alisema vifaa hivyo vimekuja muda muafaka
kwasababu wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha kwamba taarifa zote za wagonjwa zinahifadhiwa kwa njia ya Kielektoniki.

Alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakitunza taarifa za wagonjwa katika makaratasi hali inayosababisha baadhi ya taarifa hizo
kupotea au kuchelewa kupatikana pindi zinapohitajika.

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4