News Archive

Kila mwanadamu ana ndoto zake na kila siku hufikiria namna ya kuzitimiza lakini kutokana na changamoto za maisha
wengi wamejikuta wanakufa bila kuzifikia ndoto zao na hata kujikuta katika maisha duni sana baada ya kuishiwa nguvu.

Hili jambo linaumiza sana maisha ya watu wengi  ambao hawajui njia pekee ya kujilinda dhidi ya changamoto za maisha
lakini pia kujenga msingi imara wa maisha ya baadae ambapo mtu huwa dhaifu na hana  nguvu ya kufanya kazi ili  kujiingizia kipato.

Kulingana na hali hii Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzisha shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF
kwa sheria Na 28 ya mwaka 1997 kwa madhumuni ya kutoa kinga dhidi ya majanga ya kijamii yaliyo ainishwa katika azimio la Umoja wa Mataifa  Na.102 la mwaka 1952,
sheria hii iliyoanzisha NSSF ilitokana na kufutwa kwa sheria ya NPF  Na.36 ya mwaka 1964.

Mpango wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF ulianza kama idara ya Serikali mwaka 1964 kabla ya kuanzishwa kama shirika la Taifa la Akiba ya Wafanyakazi (NPF),
sheria hii iliendelea hadi Serikali ilipopitisha sheria Na. 28 ya mwaka 1997 iliyoanzisha Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF kama mpango kamili wa Hifadhi ya jamii unaozingatia kanuni za kimataifa.

Mabadiliko hayo yameiwezesha NSSF kutoa mafao mengi na bora zaidi ambayo yamegawanyika katika makundi mawili mafao ya muda mrefu na mafao ya mda mfupi,
mafao ya Muda mrefu ni Pesheni ya Uzee, Pesheni ya Ulemavu na Pesheni ya Urithi ambapo Mafao ya muda mfupi ni Mafao ya uzazi,
Mafao ya kuumia kazini na magonjwa yatokanayo na kazi, msaada wa mazishi na Mafao ya Matibabu.

Utoaji wa mafao yote hayo ni jitihada za dhati za NSSF kuhakikisha kuwa inawaondolea Watanzania changamoto za maisha na kujenga maisha yao ya baadae kwa kutoa mafao yaliyo bora na yenye tija.

Kujiunga na NSSF ni njia pekee ya mtanzania yeyote ya kujilinda kimaisha na kujenga maisha ya hapo baadaye baada ya kukosa nguvu za kujiingizia kipato na hata kutengeneza urithi ulio bora kwa familia yake.

Namna gani NSSF inaweza kulinda maisha ya mtu , NSSF hutoa mafao ya matibabu  ambayo hutolewa kwa mwanachama na wategemezi wake ambao ni mke, mume, na watoto wasiozidi wanne
wenye umri usiozidi miaka 18 au 21 lengo ni kuhakikisha wanachama wanakuwa na afya njema wakati wote wa shughuli zao.  

Hata hivyo NSSF hutoa mafao ya uzazi kwa wanawake wanaotegemea kujifungua au waliojifungua kwa kupata matibabu bure wakati wote wa ujauzito na masaa 48 baada ya kujifungua au siku 7 ikiwa atajifungua kwa upasuaji.

Kwa jitihada zake pia NSSF  hutoa mafao ya kuumia kazini, mafao haya hulipwa kwa mwanachama aliyepata ajali kazini au maginjwa yatokanayo na kazi anayoifanya,
lakini pia hutoa mafao ya msaada wa mazishi ambayo ni gharama za mazishi zilizotumiwa na wanafamilia katika kumzika mwanachama wa NSSF aliefariki.

Hivyo ndivyo NSSF humfanya mwanachama aweze kutimiza Ndoto zake za maisha bila vikwazo vya afya na changamoto zingine na kumfanya ajiamini na kufanya kazi kwa weledi na ufanisi kwa kuwa analo tegemezi la kudumu.   

Katika kujenga maisha ya baadae NSSF hutoa Pesheni ya Uzee ambapo  Mwanachama atalipwa kila mwezi ikiwa atakuwa na vigezo  mara tu baada ya kustaafu,
pesheni ya Ulemavu ambapo hulipwa kwa mwanachama aliyepoteza angalau thelusi mbili ya uwezo wake wa kufanya kazi kutokana na ulemavu wa kimwili au kiakili.

Licha ya kulinda maisha na kujenga maisha ya baadae NSSF pia hujihusisha na uwekezaji katika maeneo tofauti kwa viwango tofauti kama miradi ya ujenzi,
Hisa kwenye makampuni, Dhamana za Serikali, Akiba ya muda maalum, Dhamana za makapuni na hisa kwenye soko la mitaji.

Katika miradi ya ujenzi ambayo NSSF imefanya na imeleta maendeleo makubwa kwa taifa ni Mradi wa nyumba za mtoni Kijichi, Ujenzi wa Daraja la Kigamboni,
Ujenzi wa chuo kikuu cha UDOM, Ujenzi wa mabweni ya Chuo kikuu cha UDSM Mabibo Dar es Salaam, Ujenzi wa jengo jipya la Bunge Dodoma,
Ujenzi wa Chuo kikuu cha Nelson Mandela Arusha pamoja na miradi mingine mingi.

NSSF  hutambua kuwa mafao ni haki ya mwanachama kisheria na hulipwa moja kwa moja kwa mwanachama husika bila kupitia kwa mwajiri wake.

Na hata hivyo NSSF imeweza kujinyakulia tuzo mbalimbali za kimataifa kutokana na huduma bora ya mafao ya hifadhi ya jamii inayoyatoa kwa wanachama wake,
miogoni mwa tuzo hizo ni SSRA AWARD Tuzo hii ilipewa NSSF na mamlaka ya kudhibiti mifuko ya hifadhi ya jamii Tanzania kwa kua na ofisi nyingi zilizoenea kote nchini.

Tuzo zingine ni pamoja na Tuzo ya ushindi wa kwanza katika maonyesho ya 39  2015 ya kimataifa ya kibiashara (Sabasaba)  pia ilinyakua Tuzo hii mwaka 2010, 2012 na 2013,
PPRA AWARD Tuzo ya kutekeleza sheria ya manunuzi ya Uma iliyotolewa na mamlaka ya usimamizi ya manunuzi ya Uma na ISO 900I:2008 Tuzo ya utoaji huduma bora kwa kiwango cha kimataifa iliyotolewa na BSI February 2014.

Pia pensheni ya NSSF inatolewa kulingana na hali ya maisha kwa wakati huo hivyo hupanda na mabadiliko ya kiuchumi,  hiyo yote ni kwaajili ya kuwajali wanachama wake kulingana na mahitaji ya wakati huo

Mpaka sasa  NSSF inamtandao  mkubwa kwa lengo la kuhudumia wanachama wengi zaidi na kwa ubora wa hali ya juu,  
katika mikoa yote ya Tanzania na baadhi ya wilaya kuna Ofisi za NSSF ambazo hutoa huduma za uandikishwaji wa waajiri na wafanyakazi na ukusanyaji wa michango.

Pamoja na kuenea nchi nzima NSSF pia inatoa mafao katika Nyanja mbalimbali ambayo ni Hiari scheme, huu ni mpango mahususi ulianzishwa kwa nia ya kutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa watu walio katika sekta isiyo rasimi,
Madini Scheme kuwakinga wachimbaji dhidi ya majanga kwa kuwapa Mafao yote yatolewayo na NSSF

Nyanja zingine  ni Wakulima Scheme, hutoa mafao yote yatolewayo na NSSF kwa wanachama wa sekta ya kilimo na Wavuvi Scheme, kuwakinga wavuvi dhidi ya majanga kwa kuwapa mafao yote yatolewayo na NSSF.

Na sasa NSSF imeanzisha Mpango maalumu kwaajili ya Mwanafunzi wa vyo vikuu dhumuni ni kumwezesha Mwanafunzi kujiwekea akiba katika mfuko wa hifadhi ya jamii na kupata huduma ya matibabu bure

Mpango huo uliopewa jina la AA Plus ( Afya na Akiba kwa Wanafunzi ) umelenga pia kumuwezesha mwanafunzi kujijengea mtaji wa kujiajiri mwenyewe amalizapo masomo pamoja na kuwa na afya bora wakati wote akiwa masomoni.

Kutokana na kuhudumia watu wengi zaidi ndani ya nchi NSSF imepanua wigo na  kuvuka mipaka  kwaajili ya Watanzania waishio ughaibuni kupitia mpango maalmu ujulikanao kama WESTAD ambapo hutoa mafao ya matibabu bure,
kusafirisha mwili wa marehemu ambaye ni mwanachma, gharama za mazishi kwa mwanachama aliyechagua kuzikwa ughaibuni.   

Ili kujiunga na NSSF tembelea ofisi iliyo karibu nawe uweze kujiunga na kunufaika na huduma bora zinazotolewa na Shirika Hili la Serikali lilodhamilia kulinda na kujenga maisha ya badae ya kila mwanachama wake.

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4