News Archive

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF kwa kushirikiana na PPF limesaini makubaliano na jeshi la Magereza ya kuendeleza kiwanda cha sukari na shamba la miwa Mbigiri mkoani Morogoro.

Katika utekelezaji wa agizo hilo NSSF imejipanga kufufua kiwanda hicho cha sukari na kuzalisha zaidi ya tani 30,000 za sukari kila mwaka na kwamba tani zaidi ya 400,000 zitazalishwa katika kilimo cha miwa kwenye shamba hilo  na jeshi la   Magereza.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa  Godius Kahyaara amesema kwamba uzalishaji wa sukari nchini ninafasi nzuri kwa Tanzania kuwa nchi ya viwanda ikiwa ni moja ya ahadi ya raisi kuifanya nchi yetu kuwa na uchumi huo na kwamba kufufuliwa kwa kilimo cha miwa kitawapa fursa wakazi wa Dakawa kuuza miwa yao  kiwandani na pia itazalisha  nafasi za kazi na kupunguza umaskini miongoni mwa vijana.

Mpango huo ambao uko chini ya shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na PPF kwa kushirikiana na jeshi la Magereza imejipanga kuzalisha tani nyingi za sukari ili kuokoa fedha za kigeni ambazo hutumika kila mwaka kwaajili ya kuagiza sukari nje ya nchi.

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4