Sifa Zinazotakiwa

NSSF hutoa mafao ya pensheni ya uzee ambayo hulipwa kwa kila mwezi kwa mwanachama aliyetimiza sifa zifuatazo;

 • awe ametimiza umri wa kustaafu kwa hiari wa miaka 55 – 59 au kustaafu kwa lazima kwa miaka 60
 • awe amechangia katika mpango wa hifadhi ya jamii si chini ya michango 180
 • Kwa wanachama waliokuwa na umri mkubwa wakati NSSF inaanza wanao unafuu wa viwango vya michango inayotakiwa kama inavyooneshwa katika jedwali la hapa chini;

 uzeeni-chart 

Mafao yanayotolewa

Pensheni ya uzee hupatikana kutokana na wastani wa mapato ya mwanachama kwa miaka mitano yenye michango mizuri/mikubwa katika kipindi cha miaka kumi ya mwisho.

Kiwango cha Pensheni ya kuanzia ni 30% ya wastani wa mapato kwa mwanachama aliyetimiza michango 180. Hata hivyo 1.5% huongezwa kwa kila miezi 12 inayozidi 180 hadi kufikia kiwango cha juu kabisa cha 67.5% ya wastani wa mapato ya mwanachama.

Mafao yanayotolewa katika pensheni ya uzee ni;

 • Pensheni ya kila mwezi
 • Mkupuo wa awali kabla ya kuanza malipo ya pensheni ambao ni kiwango cha pensheni mara miezi 24
 • Mkupuo maalum kwa mwanachama aliyekosa sifa ya pensheni yaani wastani wa michango ya mwanachama kwa miezi 60 mara idadi ya michango
 • Kiasi cha chini cha pensheni ni 80% ya Kima Cha Chini cha Mshahara (KCC) unaotangazwa na Serikali
 • Kiasi cha juu cha pensheni ni 67.5% ya wastani wa mapato ya mwezi.

Kanuni ya Pensheni ya Uzeeni.

(i) Hesabu za malipo ya mkupuo

formula = (1/580 x N x APE) x 12.5 x 25%

Where:

(i)    1/580 = Accrual Factor per Month
(ii)   N = Muda wa kuchangia
(iii)  APE = Wastani wa mapato ya mwezi kwa kipindi cha miaka kumi
       (Average annual salary of the best three years out of last 10 years).
(iv)  Commutation factor = 12.5
(v)   Commutation rate = 25%

(ii) Kanuni ya Pensheni ya Malipo ya kila mwezi =

formula = (1/580 x N x APE) x 75% x 1/12

Mafao yanayotolewa.

Malipo ya kila mwezi kwa mstaafu aliekidhi vigezo.

 • Mkupuo wa awali kabla ya kuanza malipo ya penshen ambayo ni kiango cha penshen mara 12.5
 • Mkupuo maalum kwa mwanachama aliekosa sifa ya pensheni yaani wastani wa michango ya wanacham kwa miezi 60 mara idadi ya michango.
 • Kiasi cha chini cha pensheni ni 40% ya kima cha chini cha mishahara unaotangazwa na serikali.
 • Kiasi cha juu cha pensheni ni 72.5% ya wastani wa mapatoya mwaka.

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1