Pensheni ya urithi hulipwa kwa wategemezi wa mwanachama aliyefariki ambao ni mke/mume na watoto wasiozidi wanne wa chini ya umri wa miaka 18 au 21 ikiwa wapo masomoni. Iwapo hawa hawapo basi mafao yatalipwa kwa wazazi wa mwanachama aliyefariki. Kama wote hawapo atalipwa ndugu wa karibu kwa mujibu wa sheria ya mirathi.
Sifa Zinazotakiwa
Pensheni hii hulipwa iwapo mwanachama aliyefariki;
- Alikuwa ametimiza umri wa kustaafu na kuwa na sifa za kupata pensheni ya uzee baada ya kufungua madai hayo ya pensheni ya uzee.
- Alikuwa na sifa za kupata pensheni ya ulemavu ikiwa alikuwa na ulemavu wa kudumu.
Mafao Yanayotolewa
- Ukokotoaji wa pensheni ya urithi ni sawa na ule wa pensheni ya uzee isipokuwa huongezwa 1% kwa kila michango 12 inayozidi kiwango cha michango 180
- Mafao yanayotolewa pia ni sawa na mafao ya pensheni ya uzee yaani pensheni ya kila mwezi, mkupuo wa awali na mkupuo maalum kwa aliyekosa sifa zinazotakiwa.
Mgawanyo wa Pensheni ya Urithi
Mafao ya Pensheni ya urithi hugawanywa kwa kiwango cha 40% kwa mke/mume, 60% kwa watoto au 100% kwa wazazi iwapo hakuna mke/mume na watoto;