Mafao haya ni marejesho ya gharama za mazishi zilizotumiwa na wanafamilia katika kumzika mwanachama wa NSSF aliyefariki dunia.

Sifa Zinazotakiwa

 • Mwanachama aliyefariki ni lazima alikuwa akichangia kabla ya kufa kwake
 • Mwanachama aliyefariki ni lazima awe amechangia angalau mchango mmoja
 • Kuwe na gharama za mazishi zinazohusiana na mwanachama aliyefariki
 • Madai yafanyike ndani ya siku 60 baada ya kifo cha mwanachama

Gharama za mazishi zinazohusika na marejesho haya ni kama;

 • sanduku la kusafirishia mwili wa marehemu
 • uchimbaji wa kaburi
 • mashada ya maua
 • ubao wa kuzikia
 • kuni au mafuta ya kuchomea maiti (kwa wale wanaozika kwa kuchoma moto)
 • Madawa ya kuhifadhia maiti
 • Usafiri wa kwenda makaburini

Mafao yanayotolewa

Marejesho ya mafao haya hutolewa kulingana na viwango vya michango kama ifuatavyo.

maazishi

Viwango hivi hurekebishwa na Bodi ya Wadhamini ya NSSF kila inapotokea haja ya kufanya hivyo.

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1