Mafao haya hulipwa kwa wanachama wanawake wanaotegemea kujifungua au wameshajifungua.

Sifa Zinazotakiwa.

 • Awe amechangia angalau michango 36 kati ya hiyo michango 12 iwe imefanywa karibu na wiki ya kujifungua
 • Awe anategemea kujifungua au ameshajifungua mtoto
 • Hulipwa kila baada ya miaka mitatu isipokuwa ikiwa mtoto atafariki ndani ya miezi 12 baada ya kuzaliwa.
 • Madai yafanyike kabla ya kujifungua au ndani ya siku 90 baada ya kujifungua

Mafao yanayotolewa

 • Mafao ya fedha taslimu

Mafao haya ni asilimia 100% ya wastani wa mapato ya siku ya mwanachama kwa kipindi cha miezi sita kabla ya wiki ya 20 ya ujauzito. Mafao haya hulipwa kwa muda wa wiki 12, sawa na mishahara ya miezi 3.

Malipo hufanyika kwa awamu mbili yaani wiki 4 kabla ya kujifungua na wiki 8 baada ya kujifungua. Mwananchama anaweza kuamua kulipwa kwa wiki zote 12 baada ya kujifungua.

 • Mafao ya Matibabu

Matibabu hutolewa kwa magonjwa yanayoambatana na ujauzito wa mwanachama. Matibabu huanza kutolewa baada ya wiki ya 24 ya ujauzito na huishia masaa 48 baada ya kujifungua au siku 7 ikiwa kajifungua kwa upasuaji. Matibabu haya hufanywa na hospitali ambazo zimeingia mkataba na Shirika wa kutibu wanachama wa NSSF

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1