Mafao haya hulipwa kwa mwanachama aliyepata ajali akiwa kazini au magonjwa yatokanayo na kazi anayoifanya.

Sifa zinazotakiwa

 • Awe tayari alishaandikishwa na NSSF kama mwanachama
 • Awe ameumia kutokana na kazi anayoifanya au kupata magonjwa yatokanayo na kazi yake

Mafao yanayotolewa

Mafao ya fedha taslimu

 • Kwa mwanachama aliyepata maumivu ya muda, mafao yanayotolewa ni 60% ya wastani wa mapato yake ya siku. Mafao haya hulipwa kwa muda usiozidi wiki 26 tangu tarehe ya kuumia au kupata ugonjwa.
 • Kwa mwanachama aliyepata maumivu ya kudumu yaani maumivu ya 100% ya uwezo wake wa kufanya kazi, mafao yanayotolewa ni 70% ya wastani wa mapato yake ya mwezi. Malipo hufanyika kutegemea viwango vya kuumia kama vilivyoelezewa katika Kanuni za NSSF za mafao haya.

Viungo vya Bandia

Shirika hutoa viungo bandia kwa ajili ya kumsaidia mwanachama iwapo vitahitajika kama vitakavyoelezwa na Madaktari wanaohusika. Viungo hivi ni vile vinavyopatikana katika hospitali zilizopo ndani ya Tanzania

Mafao ya Kifo

Ikiwa mwanachama atafariki kutokana na ajali au ugonjwa unatokana na kazi kabla ya kufungua madai ya mafao ya kuumia kazini wategemezi wake watalipwa mafao ya pensheni ya 60% ya wastani wa mapato yake kwa mwezi.

Ikiwa wategemezi hawa watastahili pia mafao mengine yaliyo katika Sheria ya NSSF watalipwa mafao yale yatakayo kuwa ya kiwango kikubwa zaidi ya mengine.

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1