Mafao haya hutolewa kwa mwanachama na wategemezi wake ambao ni mume/ mke na watoto wasiozidi wanne wenye umri usiozidi miaka 18 au 21 ikiwa wako shuleni.

Lengo la Mafao ya Matibabu

 • Kutimiza matakwa ya kisheria kama yalivyoainishwa katika Sheria ya NSSF Na. 28 ya mwaka 1997
 • Kusaidia juhudi za Serikali katika kutoa huduma za afya kwa wananchi na hasa wanachama wa NSSF na kupunguza umaskini
 • Kupunguza gharama za matibabu kwa waajiri na wanachama wa Shirika.

Sifa Zinazotakiwa

 • Mwanachama awe amechangia angalau michango ya miezi mitatu karibu na kupata huduma za matibabu
 • Makato ya 6% ya pensheni kwa wastaafu watakaotaka kupata huduma za matibabu baada ya kustaafu.

Huduma Zinazotolewa

Huduma za matibabu zinazopatikana katika mafao haya ni kama ifuatavyo;

matibabu

Huduma za Matibabu Zilizo Nje ya Mpango wa NSSF

Huduma za matibabu zifuatazo hazitahusika katika mpango huu wa NSSF

 • Huduma za matibabu zilizo chini ya mafao ya uzazi
 • Huduma zilizo chini ya mpango wa Taifa wa Serikali kama huduma za mama na mtoto, chanjo, kifua kikuu na ukoma, VVU/Ukimwi, saratani, magonjwa ya mlipuko, kisukari, n.k.
 • Matibabu/Huduma za kujitakia kama athari za ulevi, madawa ya kulevya, matumizi ya sigara, majaribio ya kujiua na utoaji mimba usio halali
 • Magonjwa ya akili isipokuwa kwa kipindi cha mlipuko/kupata kichaa siku 7 za mwanzo)
 • Uchunguzi wa gharama kubwa kama MRI na DNA au yoyote inayozidi viwango vilivyowekwa na Shirika
 • Athari za matukio ya kushiriki katika mikusanyiko isiyo halali kama maandamano, migomo, n.k
 • Huduma za uchunguzi kwa ajili ya safari, ajira au shule
 • Huduma za mama cheza majumbani
 • Matibabu yanayotokana na majaribio ya dawa

Mipaka Katika Mafao ya Matibabu

Katika kutoa huduma za matibabu chini ya mafao ya matibabu, Shirika limeweka mipaka ifuatayo;

 • Kulazwa ni kwa siku 42 kwa mwaka kwa familia
 • Matibabu ya dharura nje ya vituo/hospitali alichojiandikisha kwa wanachama wanachama wanaosafiri kikazi si zaidi ya mara nne kwa mwaka kwa wagonjwa wa nje na si zaidi ya masaa 48 mara mbili kwa mwaka kwa wagonjwa wanaolazwa.

Uandikishaji

Mwanachama anawajibika kujiorodhesha mwenyewe pamoja na familia yake katika ofisi ya NSSF iliyokaribu nae. Atawajibika pia kuchagua hospitali ambayo anapenda kutibiwa kwa mwaka mmoja katika orodha ya hospitali zilizoingia mkataba na Shirika.

Katika kujiorodhesha mwanachama anawajibika kuonyesha au kuwasilisha kadi yake ya uanachama, cheti halisi cha ndoa iwapo ameoa/olewa, vyeti halisi vya kuzaliwa watoto kama wapo na picha za pasipoti za wahusika wote.

Kukoma kwa Huduma za Matibabu

Huduma za matibabu katika mpango huu zinaweza kusitishwa mara moja kutokana na mambo yafuatayo;

 • Kifo cha mwanachama
 • Kuachishwa au kuacha kazi
 • Kustaafu kwa umri
 • Kutowasilishwa kwa michango kwa zaidi ya kipindi cha miezi mitatu.
 • Kufikia umri wa zaidi ya miaka 18 au 21 kwa watoto

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1