Mpango wa Taifa wa hifadhi ya jamii wa NSSF unahusika na wafanyakazi wote walio katika sekta binafsi, walioajiriwa na Serikali au Makampuni ya
umma, Mashirika au Taasisi zisizo za kiserikali na Ofisi zote za Balozi zinazoajiri watanzania.

Uandikishaji Waajiri

Waajiri wanaohusika kisheria kuandikishwa katika mfumo wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF ni;

 • Waajiri wote walio katika sekta binafsi
 • Taasisi zisizokuwa za kiserikali
 • Ofisi za Kibalozi zinazoajiri Watanzania
 • Taasisi za Kimataifa zinazofanya shughuli ndani ya Jamhuri ya
 • Muungano wa Tanzania
 • Taasisi na Wizara za Serikali
 • Mashirika ya Umma
 • Watu binafsi waliojiajiri wenyewe
 • Sehemu yoyote ya shughuli kama itakavyotangazwa na Waziri anayehusika na kazi

Muda wa Kujiandikisha

Mwajiri yeyote anawajibika kujiandikisha katika shirika kama mwajiri mlipa michango na kupewa namba ya uandikishaji mara tu anapoanza shughuli
zake.

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4

Login Form1