News Archive

Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya kiasi cha shilingi Trilioni kwa mwaka na kwamba wafanyakazi wazembe hawatovumiliwa.

 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF William Erio katika mkutano wake na Wakurugenzi na Mameneja uliofanyika katika ukumbi wa NSSF Ilala jijini Dar es salaam na kusema kwamba lazima Shirika lifikie malengo makubwa .

“Mwaka jana tulipaswa kukusanya shilingi trilioni moja , lakini tukakusanya Bilioni 750 tu hivyo sasa tunatakiwa kuhakikisha zinafikia zile zinazohitajika”alisema Erio.

Baadhi ya Wakurugenzi, Mameneja na Wafanyakazi wa NSSF wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu kwenye ukumbi wa mikutano Ilala mafao House

Erio amewataka wafanyakazi kuhakikisha wanashawishi wananchi kujiunga na mfuko wa NSSF ili kuongeza idadi kubwa ya wanachama ambapo amesema mwaka huu tunatakiwa kusajili wanachama wapya 417,000, na kwa kuwa NSSF ina wafanyakazi zaidi ya 1000 endapo kila mfanyakazi akileta mwanachama mmoja shirika litakuwa na wanachama wengi.

“Mbali na kuandikisha wanachama pia kuna swala la wanachama hao wapya kuanza kuwasilisha michango yao ili kuwa wanachama hai, haina maana kuwa na wanachama wengi ambao sio wachangiaji”, Alisema Erio.

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4