News Archive

MWELEKEO mpya wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF katika sekta isiyo rasmi  ndio umeanza kushika kasi kwa sasa  ambapo wananchi mbali mbali wanatarajiwa kupata faida nyingi katika maisha yao ya sasa na  ya baadae.

Hii imetokana na kwamba kwa sasa NSSF ndio mfuko pekee unaohudumia sekta isiyo rasmi , na hii ni kwa mujibu wa sheria namba mbili ya Bunge ya mwaka 2018 ambapo Shirika limepewa nguvu ya kufanya kazi hiyo.

 

Sekta isiyo rasmi ni sketa ambayo inajumuisha watu mbali mbali ambao wamejiajiri wenyewe katika mifumo ya ajira isiyorasmi ambayo kwa kiwango kikubwa inajumuisha watanzania wengi na wa matabaka mbali mbali.

Takwimu za ajira za  mwaka 2017/2018 zinaonyesha kuwa ni Watanzania 2.3 (11.6%)  Walioajiriwa katika sekta rasmi  ikilinganishwa na Waliojiajiajiri katika Sekta Isiyo rasmi ambao ni  milioni  18.4 m (88.4 ambapo sasa ndio sababu shirika linasisitiza wananchi wasio kwenye sekta isiyo rasmi ni wengi na wanapaswa kujiunga katika mfumo wa Hifadhi ya Jamii ili kufaidika na mafao yanayotolewa.

Waliomo katika sekta hii ni kama vile, wajasiriamali, wafanyabiashara Mama Lishe,Mvuvi,Dereva boda boda, Mkulima, Msusi, Mmachinga na  mwanamichezo ambao kwa namna moja ama nyingine hawa hujiajiri wenyewe katika kuendesha maisha yao tofauti na wafanyakazi wanaoajiriwa katika sekta iliyo rasmi.

Akizungumza wakati wa semina mbalimbali za kwa viongozi wa Vikundi Mwenyekiti wa kuratibisha Hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi Bi. Maryam Muhaji alisema Shirika la NSSF  sasa imeamua kuweka nguvu kwa ajili ya kuhakikisha wananchi walio katika sekta isiyo rasmi wanaweza kufaidika na mfuko huu kwa kupata mafao mbali mbali.

Mwananchi ambaye yupo katika sekta isiyorasmi akiwa mwanachama wa NSSF  atafaidika na  matibabu bure yeye  pamoja na mwenza wake na watoto wa nne baada ya kuchangia kwa miezi mitatu ambapo kima cha chini ni  shilingi elfu ishirini kwa kila mwezi. Na endapo ataweka akiba kwa muda wa miaka kumi na mitano  atapata pensheni ya uzeeni iwapo atakuwa amefikisha umri wa miaka 55 au 60 

Hii ndio sababu sasa shirika linaendelea kuhamasisha wananchi ambao wako kwenye mfumo wa sekta isiyo rasmi kuweza kujisajili na kuwa kwenye mfumo rasmi wa kuweka akiba na baadae kufaidika na mafao mbali mbali yanayotolewa.shirika linafanya maboresho mbalimbali katika mafao ya matibabu ambapo Mwanachama ataruhusiwa kubadilisha hospitali kila baada ya miezi mitatu, Mwanachama ataruhusiwa kupata huduma za matibabu pale atakapokuwa nje ya mkoa wake mara sita (6) kwa mwaka, Kutakuwa na maduka ya dawa yatakayo sajiliwa na shirika kwaajili ya kusadia kutoa huduma za dawa na Shirika litasajili vituo vinavyo toa huduma za matibabu vijijini na kuvipatia mikopo kwa ajili ya kuboresha huduma za matibabu..

Vile vile iwapo mwanachama mwanamke ataweka akiba kwa muda wa miaka mitatu na iwapo atapata ujauzito na kujifungua atalipwa mafao ya uzazi ambayo ni asilimia 300 ya kipato chake cha mwezi. Michango 12 ya mwisho shurti iwe imechangiwa  kipindi cha ujauzito.

Vilevile mwanachama atakapopoteza uwezo wake wa kufanya kazi kwa kiwango cha ¾ atalipwa mafao ya ulemavu kwa kipindi chote kabla ya kufika miaka sitini na atakapofika umri wa miaka 60 atalipwa mafao ya uzeeni na kama mwanachama atafariki wategemezi wake watalipwa mafao ya urithi.

Baadhi ya wananchi ambao hawako katika  sekta rasmi ya ajira wanasema wameona ni jambo la muhimu na lenye  faida kwao kujiandikisha na kufaidika katika mafao yanayotolewa  na mfuko, huku wakiwapa wito wananchi wengi zaidi kujisajili. Shirika limeendela kutoa elimu kwa wanachi juu ya umuhimu wa kujiandikisha, jambo ambalo linaendelea kupokelewa vizuri kwani wengi wamejiandikisha kwa ajili ya kujiwekea akiba ya uzeeni na kupata matibabu bure

Mbali na hayo mwanachama atafaidika na mikopo mbalimbali inayotolewa na NSSF kupitia mabenki, hapo siku za nyuma NSSF ilikuwa ikitoa mikopo ya aina hiyo lakini kwa sasa wameamua kuipitia upya ili iweze kuwafikia wanachama wengi zaidi na kuongeza ufanisi katika kuitoa na kuifuatilia mikopo hiyo.

NSSF imeshaingia mkataba na Benki ya Azania ili wanachama waweze kupata mikopo ya NSSF Kupitia benki Hiyo, vile vile NSSF ipo katika hatua mbalimbali za majadiliano na Benki nyingine nchini ili kuhakikisha mikopo hiyo inawafikia wanachama wote wa mijini na vijijini.

Zamani swala la hifadhi ya jamii lilikuwa limewalenga sana waajiriwa na  likiwachaa nje waliojiajiri wenyewe na hivyo kukosa mambo muhimu sana  ikiwemo kinga za majanga kama vile Pensheni ya uzee na mafao mengine muhimu kama matibabu na mafao ya uzazi . Sababu kubwa ni pamoja na mfumo uliokuwepo uliokuwa unaweka msisitizo kwa walioajiriwa tu kuwa katika hifadhi ya jamii wakati walioajiriwa katika nchi hii ni wachache sana ukilinganisha na wale waliojiajiri wenyewe.

Bi. Maryam Muhaji aliongeza kwa kusema,semina za kuelemisha viongozi wa Vikundi na wajasiriamali zilianzia mkoani mara,Mwanza, bukoba, na kwa sasa zinaendela katika mikoa ya Arusha, Moshi na Tanga na semina hizoi  zinatarajiwa kuwa endelevu katika maeneo yote nchini

Katika Juhudi za kuiunga mkono mpango huu,  Viongozi mbali mbali  wa serikali wameendelea kushiriki katika uhamasishaji wa vikundi wakati wa semina katika mikoa yao . Akizungumza katika uzinduzi wa semina ya viongozi wa vikundi vya uzalishaji mali mkoani Kilimanjaro  Mkuu wa wilaya  ya Moshi Mhe Kipi Warioba alisema mpango huu ni habari njema kwa watu wa Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla kwa sababu mitaji ya biashara imekuwa ni changamoto kubwa sana pale watu wakitaka kuanzisha shughuli yoyote ya kujiongezea kipato na aliwasisitiza viongozi wa Vikundi kuwafikishia habari hii wanachama wa vikundi vyao haraka sana ili kufanikisha lengo la Mpango huu wa NSSF.

Alisema Serikali inaunga mkono mpango huu wa  NSSF  kwa asilimia mia moja kwani utasaidia kupunguza umaskini kwa kuwasaidia wanachama kujiongezea kipato kupitia biashara ndogo ndogo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela alisema Serikali ya  awamu ya Tano ni serikali makini inayomjali  kila mtu na hasa watu  wa hali ya kipato cha chini.Kwa kutambua umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa wote  Bunge sasa limepitisha sheria mpya namba 2 ya mwaka 2018  inayoboresha hifadhi ya jamii nchini ambapo Sheria hiyo imeacha mifuko miwili tu ambayo ni PSSSF na NSSF.

Katika mambo muhimu yaliyo katika sheria hiyo ni pamoja na msisitizo uliowekwa wa kupatinua wigo wa hifadhi ya jamii kwakuwafikia watanzania wote ikiwemo waleo waliojiajiri wenyewe yaani sekta isiyo rasmi ambapo Shirika la NSSF ndilo lililopewa Jukumu la kuhakikisha hifadhi ya Jamii inawafikia watu wote wa sekta isiyo rasmi.

Mmoja wa wafaidika wapango huu wa kujiunga kwa Hiari ni Mkazi wa Dar es salaam Peter Nyema ameelezea kuhusiana  na hatua hii ya wananchi ambao wamo katika sekta isiyo rasmi kuwa ni mpango mzuri amabo unasaidia wananchi waliojiajiri kunufaika na mafao “ Huu mpango wa kujiunga kwa Hiari ni mzuri sana, mimi na familia yangu tumefaidika nao “ alisema Nyema.

 

 

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4