News Archive

Waziri Mkuu Majaliwa alitoa pongezi hizo mkoani Morogoro Septemba 4, 2017 mara tu baada ya kuongoza zoezi la upandaji wa miwa ikiwa ni ishara ya kuunga mkono mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari unaofahamika kama Mkulazi II unaotekelezwa kwa ubia kati ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF kupitia kampuni Hodhi ya Mkulazi Holding unaofanyika katika gereza la Mbigiri, Dakawa mkoani Morogoro.
Akizungumzia mradi huo Waziri Mkuu alisema pamoja na kumaliza tatizo la uhaba wa sukari hapa nchini, pia utapunguza tatizo la ajira sambamba na kukuza uchumi wa nchi.

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) pamoja na Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama  (katikati) wakiongoza zoezi la upandaji wa miwa ikiwa ni ishara ya kuunga mkono mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari unaofahamika kama Mkulazi II unaotekelezwa kwa ubia kati ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na PPF kupitia kampuni Hodhi ya Mkulazi Holding unaofanyika katika gereza la Mbigiri, Dakawa mkoani Morogoro. Kulia, akishirikiana nao ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe


Ili kuhakikisha wananchi wanakuwa kwenye nafasi ya kushiriki kikamilifu katika kuzalisha malighafi kwa ajili ya kiwanda hicho Waziri Mkuu aliutaka uongozi wa mkoa huo kuhakakikisha wanapita wilaya nzima ya Kilosa unapotekelezwa mradi huo kuhakikisha hakuna mashamba pori zoezi litakaloambatana na unyang'anyaji wa mashamba yasiyoendelezwa kutoka kwa wamiliki wake na kisha kukabidhiwa kwa wananchi wayatumie kwa kilimo.


Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji , Charles Mwijage alisema lengo la serikali ni kuhakikisha taifa linazalisha sukari tani milioni mbili ili lijitosheleze na kuuza nje ya nchi ambapo kwa sasa licha ya mahitaji ya sukari kuwa ni tani 600,000 taifa linazalisha takribani laki tatu.


Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio, walihakikishia serikali, wanachama na wadau wote wa mifuko hiyo kuwa utekelezaji wa mpango huo pamoja na mambo mengine unalenga kuongeza ajira na kupunguza kabisa kasi ya mfumuko wa bei kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo muhimu.


Prof Kahyarara alisema kuwa tayari mkandarasi wa kufunga kiwanda hicho ameshapatikana wakati zoezi la upandaji wa miwa likiendelea. Lengo ni kupanda ekari 3000  za miwa ifikapo Disemba mwaka huu zoezi ambalo tayari limetoa ajira zaidi ya 150 kwa wakazi jirani na eneo la Mbigiri na wengine kutoka mikoa jirani. Prof Kahyarara  aliongeza kuwa mradi huo pia utazalisha umeme Megawatt 8.

Naye Kamishna Jenerali wa Magereza Dk Juma Malewa alisema ufufuaji wa kiwanda hicho kilichosimamisha uzalishaji wake katikati ya miaka 1990 mbali na kuwa mchango mkubwa kwa jeshi hilo pia utatoa fursa kwa wafungwa watakaoonyesha uwezo mkubwa katika utekelezaji wa mradi kuweza kupewa nafasi ya kutumikia kiwanda hicho hata baada ya kumaliza vifungo vyao.

Frequently Asked Questions

 • Nawezaje kuwa mwanachama wa NSSF? +

  Tafadhali fika katika ofisi yoyote ya NSSF iliyo karibu yako kwa zoezi la uandikishaji ukiwa na picha moja ya passport Read More
 • Napataje taarifa ya Michango yangu? +

  Kupata taarifa ya Michango, unafanya ifuatavyo : a) Sajili Tuma neno sajili,acha nafasi, weka namba yako ya uanachama. Tuma kwenda namba Read More
 • Je nifanyeje endapo michango yangu haionekani katika taarifa za akaunti yangu? +

  Tafadhali fika ofisi ya NSSF iliyo karibu nawe ili kujua sababu ya kutoonekana kwa michango yako na kuelekezwa utaratibu wa Read More
 • Je narekebishaje michango yangu? +

  Michango ya mwanachama itarekebishwa kulingana na sababu zinazopelekea kutoonekana kwa michango hiyo katika taarifa ya michango. Ofisi husika itakupa muongozo zaidi. Read More
 • Je mwanachama anayesafiri anaweza kumwachia mtu au ofisi imfatilie madai na kuchukua malipo yake?? Kwa utaratibu gani?? +

  Ndio, mwanachama anaruhusiwa kwa kujaza fomu za mandate (NSSF 22) zilizothibitishwa na mwanasheria na kufata taratibu zote za kisheria zilizoainishwa Read More
 • 1
 • 2
 • 3
 • 4